Tuesday, June 14, 2011

RAIS KIKWETE KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUZALIWA UPYA SUDAN KUSINI!

Rais JAKAYA KIKWETE amealikwa kuhudhuria sherehe za kuzaliwa kwa taifa jipya la Sudan ya kusini Sherehe zitakazofanyika Mjini Juba,Julai 9 mwaka huu.

Mwaliko huo umetolewa na mjumbe maalum wa Rais wa taifa hilo jipya Dakta CIRINO HITENG OFUHO ambae pia ni waziri wa Nchi ofisi ya Rais wa Sudan ya Kusini wakati alipokutana na Rais KIKWETE katika Ikulu ya Mjini DSM.
Akizungumza mara baada ya kupokea mwaliko wa kuhudhuria sherehe hizo Rais KIKWETE amesema tukio hilo lina umuhimu mkubwa katika historia ya Sudan ambapo pia aliwataka marais SALVA KIIR pamoja na OMAR AL-BASHIR kuendeleza hali ya utulivu nchini humo.
Aidha, Sudan Kusini imesema kuwa imedhamiria kuchukua kila hatua kuhakikisha kuwa inadumisha amani na utulivu na nchi ya Sudan ambako taifa hilo jipya litameguka.

No comments:

Post a Comment