Wednesday, June 15, 2011

TANZANIA YATAJWA KUWA YENYE CHANGAMOTO YA WATOTO WA MITAANI!

Tanzania imetajwa kuwa ni nchi mojawapo zilizopo Barani Afrika ambayo ina changamoto kubwa ya ongezeko la watoto wanaoishi mitaani na kuomba omba barabarani kutokana na sababu mbalimbali zinazofanya watoto hao kukosa haki zao za msingi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia na watoto Bi TUKAE NJIKU wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika hapo kesho.
Amesema ongezeko hilo la watoto wanaoishi mitaani hasa katika maeneo ya mijini unatokana na ukatili uliokithiri unaofanyika nyumbani na mashuleni ,kuvunjika kwa ndoa pamoja na ukosefu wa upendo katika familia nyingi nchini.
Aidha Bi TUKAE ametoa onyo kwa baadhi ya wamiliki wa vituo vya kulelea watoto yatima nchini ambao hawajasajili vituo vyao mpaka sasa ,hawana budi kufanya usajili kwani hatua za kisheria zinaweza kuchukuliwa dhidi yao.

No comments:

Post a Comment