Serikali imekiri kwamba Suala la vitendo vya Rushwa bado limendelea kuwa kikwazo kikubwa katika kufikia dhana ya utawala Bora licha ya jitihada za makusudi zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kukabiliana na tatizo hilo hapa nchini.
Hayo yamebainishwa jijini DSM na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora MATHIAS CHIKAWE wakati akifungua kongamano la mwaka la wadau wanaojihusisha na mapambano dhidi ya Rushwa vikiwemo vyombo vya habari.
Waziri CHIKAWE amesema pamoja na Serikali kuipa uwezo mkubwa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU lakini bado kuna changamoto ya kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu madhara yatokanayo na Suala la Rushwa.
Katika hatua nyingine baadhi ya washiriki wa mkutano huo wameonesha wasi wasi wao kuhusiana na vita dhidi ya rushwa inavyoendeshwa ambapo kutokana na hali hiyo wameishauri serikali kuweka msukumo zaidi katika kukabiliana na vitendo hivyo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment