Monday, June 27, 2011

SERIKALI KUENDELEA KUPELEKA FEDHA KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO-PINDA!

Waziri mkuu wa MIZENGO PINDA, amesema Serikali itaendelea kupeleka fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo vijijini sanjari na hatua hiyo pia amevitaka vyama vya siasa nchini kusaidia kuhamasisha Wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za Maendeleo.

Akijibu swali Bungeni mjini Dodoma Waziri PINDA amesema kuwa ushirikishwaji wa Wananchi katika maendeleo haimaanishi kuwa wanashurutishwa bali ni wajibu wao kushirikiana na Serikali katika utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya ki-maendeleo.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge,WILLIAM LUKUVI , amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo Serikali imeazimia kupunguza gharama za matumizi yake lengo ikiwa ni kuzipeleka fedha hizo katika miradi ya maendeleo ya wananchi.

No comments:

Post a Comment