Tuesday, June 28, 2011

Serikali imesema ipo tayari kuwalipa fidia wanachi wa Kibiti ambao nyumba zao zimebomoka kutokana na kupitishwa kwa mkongo wa mawasiliano katika makazi yao iwapo nyumba hizo zitabainika zipo nje ya Hifadhi ya Barabara.
Naibu Waziri wa Mawasiliano Charles Kitwanga amebainisha hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa kibiti Abdul Maromba wa CCM aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali kuhusu kuwalipa fidia wananchi ambao nyumba zao zimebolewa kutokana na kupitishwa kwa mkongo wa mawasiliano katika maeneo yao.
Akijibu swali hilo Naibu waziri huyo amesema Sanjari na Serikali kutaka kuwafidiwa wakazi hao pia hakuna madhara ya Ki- Afya ambayo wananchi watayapata kutokana na mkongo huo kupitishwa karibu na makazi yao.

No comments:

Post a Comment