Jumla ya Walemavu wa ngozi Albino 80 mkoani Shinyanga wamepatiwa huduma ya kupima macho bure kufuatia tatizo linalowakabili la kutoona vizuri.
Afisa Mradi wa mfuko wa elimu uliofadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la UNDER THE SAME SUN, GAMALIELI BOYA amesema shirika hilo limeamua kutoa vifaa mbalimbali vya kusaidia kuona vizuri kwa walemavu hao wa ngozi ili wakabiliane na tatizo hilo.
Baadhi ya Vifaa vilivyotolewa na shirika hilo kupitia mfuko huo wa elimu ni miwani ya jua na lenzi mbinuko zitakazowasaidia kukuza maandishi madogo yaliyopo kwenye karatasi.
Kwa upande wake RAYMOND MGANYIZI ambaye ni mmoja ya walemavu wa ngozi licha ya kushukuru amesema wamefarijika kwa shirika hilo kutambua mahitaji ya walemavu hao hasa kwa kuwapatia vifaa vya kuwasaidia kuona na kusoma Vizuri.
No comments:
Post a Comment