JOYCE CHONJO
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) limewadhamini wajasiriamali zaidi ya 100 wanaofanya shughuli mbalimbali za kiuchumi katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya SABASABA, ili kupata fursa ya kuonyesha bidhaa kwa umma ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji (NEEC) Dokta Joyce Peters Chonjo amesema lengo la udhamini ni kuwapatia fursa wajasiriamali wa ndani kutoka katika kongano mbalimbali ili kuwawezesha kufanikiwa katika upatikanaji wa masoko na taarifa.
Aidha Dokta Joyce ameongeza kuwa sera ya Uwezeshaji Wananchi kiuchumi inalenga kuondoa vikwazo ambavyo vinawazuia wananchi kushiriki katika kukuza uchumi wa nchi na kutoa nafasi zaidi kwa makundi mbalimbali kushiriki kikamilifu.
No comments:
Post a Comment