Monday, June 27, 2011

MBEYA CEMENT WAADHIMISHA SIKU YA USALAMA SEHEMU ZA KAZI!

Kampuni ya Mbeya Cement kwa kushirikiana na Kampuni ya Lafarge, wameadhimisha mwezi wa usalama sehemu za kazi na viwandani kwa ujumla, ambapo katika kampeni ya mwaka huu wametilia mkazo katika masuala ya usalama wa barabarani, ili kuhakikisha kuwa ajali za barabarani hazitokei kabisa, kwa kutoa elimu kwa madereva wa magari na jamii pia.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Lafarge Bw Mbuvi Ngunze, aliyekuwa akizungumza katika maadhimisho hayo jijini dare s salaam, amesema wamekuwa na mafanikio makubwa huku akitolea mfano kwamba hakuna ajali yoyote iliyotokea katika usafirishaji wa saruji. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka hapa nchini, ni ‘’Kuwa mjanja Kuwa salama’’.

No comments:

Post a Comment