IGP SAID MWEMA
Jeshi la polisi mkoani Singida linawashikilia wakazi wa wawili wa Majengo kwa tuhuma za kuwabaka watoto sita wa kike wa umri kati ya miaka mitatu hadi tisa.
Kamanda wa polisi mkoani humo Celina Kaluba amesema watuhumiwa hao walikamatwa jana, baada polisi kupata taarifa za kina kutoka kwa raia wema.
Amewataja wanaoshikiliwa na Jeshi hilo kuwa ni Khalfan Shaban Mwenye Umri wa miaka 21 Pamoja na Issa Juma mwenye umri wa Miaka 15 wote wakiwa ni wakazi wa Majengo, ambao wanadaiwa kuwabaka watoto hao kwa nyakati tofauti mwezi machi na juni, mwaka huu.
Amesema watoto waliobakwa ni wanafunzi darasa la pili shule ya msingi Lighwa Wilayani Singida, huku mtuhumiwa wa pili Issa akidaiwa kumbaka mtoto wa umri wa miaka mitatu ambae jina lake limehifadhiwa kwa sababu maalum yeye akiwa ni mkazi wa kibaoni.
Kamanda Kaluba amesema watuhumiwa hao wanatarajiwa kupandishwa kizimbani wakati wowote kujibu mashitaka yanayowakabili.
No comments:
Post a Comment