Watumiaji wa mitandao ya mawasiliano nchini wameongezeka na kufikia Idadi ya watu millioni 5 licha ya makampuni yanayotoa huduma hizo kukabiliwa na changamoto mbalimbali likiwemo suala la miundo mbinu hapa nchini.
Akifungua mkutano wa wadau wanaojishugulisha na masuala ya mitandao Barani Afrika Jijini DSM Katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dakta FLORENCE TURUKA amesema Watanzania bado wanayo fursa ya kujifunza namna kutumia mitandao ya mawasiliano.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Profesa JOHN NKOMA amesema pamoja na idadi ya watumiaji wa mitandao kuongezeka kwa kasi lakini bado changamoto za matumizi mabaya ya mitandao hiyo ikiwemo uhalifu.
No comments:
Post a Comment