Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE amewataka Viongozi na Watendaji wakuu wa Serikali Kutokaa Ofisini na Kusubiri kuletewa Taarifa na Badala yake watoke na kutekeleza majukumu yao nje ya Ofisi kwa kufanya ziara zenye tija kwa maendeleo ya Taifa.
Akizungumza mjini Dodoma katika semina elekezi kwa Viongozi na watendaji wa Serikali Rais KIKWETE amesema kuna Viongozi na watendaji ambao wamekuwa wakikaa Ofisini na kuandika madodoso ama kusubiri kupokea Taarifa hali inayosababisha kupatiwa taarifa za uongo kutoka kwa watendaji wa Chini NA KUWATAKA kudhibiti matumizi ya feha za serikali...
Rais KIKWETE amesema ili Tanzania ifikie lengo hilo ni lazima msukumo uwekwe katika upatikanaji wa huduma za kijamii ambazo kwa sasa hazitoshelezi na kubainisha kuwa mpaka sasa ni asilimia 14 tu ya watanzania ndio wanapata huduma ya umeme lengo ikiwa ni kufikisha asilimia 30 kwa miaka 5 ijayo.
No comments:
Post a Comment