Wednesday, March 21, 2012

WAFANYABAISHARA SOKO LA MCHIKICHINI WALALAMIKIA UONGOZI WAO KUDAIWA MILIONI 23 ZA UMEME!

Baadhi ya Wafanyabiashara wa Soko la Mchikichi jijini Dar es Salaam wameulalamikia uongozi wa soko hilo kwa kushindwa kulipa deni la umeme la kiasi cha shilingi Milioni 23 kwa Shirika la Umeme nchini Tanesco.



Wakizungumza na kituo hiki wafanyabiashara hao wamesema ni zaidi ya wiki moja sasa tangu Tanesco ilipokata umeme sokoni hapo bila kupewa taarifa yoyote jambo walilotaja kuwadidimiza kiuchumi. Katika hatu nyingine wafanyabiashara hao wametoa siku saba kwa uongozi wa soko hilo kumaliza tatizo hilo na kuiomba serikali kuingilia kati suala hilo ili kuepusha hasara zaidi kwa siku za usoni.

No comments:

Post a Comment