Wednesday, February 22, 2012

TUNDU LISSU AWATUHUMU POLISI KUVAMIA MAKAZI YA WANANCHI WA SINGIDA MASHARIKI!

ASKARI wa Jeshi la Polisi nchini wametuhumiwa kwa kuvamia makazi ya wananchi wa jimbo la Singida Mashariki na kuwapiga. Mbali na Jeshi hilo kuwapiga wanacnchi hao pia zaidi ya wananchi 10 wamefikishwa katika vituo vya polisi na kuwafunguliwa mashtaka.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu amesema Jeshi hilo limefikia hatua hiyo kwa lengo la kuwaondoa wananchi hao katika makazi yao ili wasiendelee na uchumbaji wa madini katika eneo hilo.


“Mwaka 2004 Kampuni ya Shanta Miningi ilipewa kibali cha kutafiti nadini katika eneo hilo,lakini pia Kanpuni hiyo ndiyo inayofanyakazi ya kuchimba madini kwa kukwepa kodi na imesajiliwa nchini Uingereza”alisema Lissu.
Hata hivyo Lissu alisema kitendo cha Jeshi la Polisi kuendelea kutesa wananchi katika jimbo hilo lililopo katika kijijini cha Mag’onyi kata ya Mag’onyi katika jimbo langu ni kukiuka haki za raia. Katika hatua nyingine Mbunge huyo alimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema kusitisha haraka zoezi hilo la kuwahamisha wananchi kwa nguvu katika eneo hilo.


“Namtaka IGP Mwema aondoe askari wake haraka katika eneo hilo,ili asije akastaafu kwa sifa mbaya kama aliyokuwa nayo IGP mstaafu Omary Mahita ya kuuwa watu kule Bulinkuru”alisema Lissu.

No comments:

Post a Comment