Wednesday, February 22, 2012

WANNE WAUAWA KIKATILI MKOANI RUVUMA WAKATI JESHI LA POLISI LIKITAWANYA MAANDAMANO KUELEKEA KITUO KIKUU CHA POLISI!

Askari wakimdhibiti mmoja wa vijana walioandamana mjini songea leo, wakipinga kitendo cha wenzao kuawa na watu wasiojulikana. Mpaka sasa inadaiwa Watu wanne wameshauawa kwenye maandamano hayo. (PICHA NA MUHIDIN AMRI).

             Polisi wakiondoa magogo yaliyokuwa yamewekwa na waandamanaji mjini Songea leo.
                                                     Askari wakiondoa mkokoteni barabarani
Polisi wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi baandhi ya vijana walioandamana mjini Songea leo kuishinikiza Serikali kufanya uchunguzi wa haraka wa vifo vya watu wanaouawa na watu wasiojulikana ambapo inadaiwa kuwa baadhi ya maiti zinapatikana zikiwa zimenyofolewa sehemu za siri.
 
Na Mwandishi Wetu
WATU wanne wameuwa kikatili na Jeshi la Polisi baada ya jeshi hilo kushindwa kuwadhibiti waandamanaji waliokuwa wakielekea katika Kituo Kikuu cha Polisi Songer na katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.



Jeshi hilo limefanya mauji ya kutisha Mkoani Ruvuma wakati ambapo zoezi la kuwatawanya waandamananji waliokuwa wakiandamana kwa lengo la kuishinikiza serikali isitishe mauaji yanayoendelea katika Mkoa huo.


Kwa muujibu wa taarifa mbalimbali ni kwamba mpaka hivi sasa watu 10 wameshachinjwa na kuuawa katika matukio mbalimbali huku wengine wakinyofolewa sehemu zao za siri. Hali hiyo ilianza kujitokeza majira ya asubuhi ambapo wakazi wa mtaa wa Lizaboni wakiandamana kuelekea katika kituo hicho cha polisi kilichopo karibu na Uwanja wa Majimaji mjini hapa.


Hata hivyo katika mapambano hayo ilidaiwa kuwa mbali na waandamanaji wanne kuuwawa pia watu 37 walidaiwa kujeruhiwa huku vurugu hizo zikisababisha uzalishaji mali na masuala mengine ya kijamii kusimama.


Katika hatua nyingine taarifa zilizotolewa na Jeshi la polisi ilidai kuwa waliokufa ni wawili katika tukio hilo na majeruhi kumi, uongozi wa hospitali ya mkoa umeweka wazi kwamba maiti zilizopokelewa katika hospitali hiyo ni nne na majeruhi 41 huku Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pia ukisema kwamba waliokufa ni wawili na majeruhi 20.


Hata hivyo mpaka tunapandisha habari hewani taarifa kamili juu ya hali hiyo ya sintafahamu ya mauaji ya raia wasiokuwa na hatia huku wengine wakipata majeraha yakutisha katika maeneo mbalimbali ya miili yao ilikuwa haijajulikana. HBARI KWA HISANI YA MTANDAO WA JAPO NEWS!

No comments:

Post a Comment