Tuesday, October 4, 2011

WANANCHI WAFAIDIKA NA HUDUMA ZA BURE ZA MATIBABU YA AFYA KATIKA MAONESHO YA MIAKA 50 YA UHURU YA UTOAJI HUDUMZA ZA AFYA TANZANIA!

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiingia katika eneo kunakotolewa huduma mbali mbali za upimaji wa afya na matibabu katika mabanda ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yaliyopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru katika utoaji huduma za afya Tanzania.(Picha na zote na mo blog)
Lucas Chagula kutoka Bohari Kuu ya Dawa Tanzania akitoa dawa kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la bohari hiyo baada ya kupima Afya zao.
Wafanyakazi wa Banda la Bohari Kuu ya Dawa kutoka kushoto ni Rehema Shelukindo, Lucas Chagula, Terry Edward na Gendi Machumani wakiwa wamekaa imara kabisa kutoa huduma kwa wananchi.
Katika Banda la Ushauri Nasaha na Upimaji VVU lililopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Muuguzi Mshauri Rehema Kessy akitoa maelekezo sahihi ya jinsi ya kutumia mipira ya kiume Kondom kwa kijana Frank Christopher.

No comments:

Post a Comment