Sunday, August 28, 2011

WAKAZI WA KIJIJI CHALA CHALA WAGOMEA KUCHANGIA UJENZI WA ZAHANATI KUSHINIKIZA ALIYEKULA FEDHA KUWAJIBISHWA!


Wakazi wa kijiji cha Chala kilichopo wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa wamesema kuwa hawataendelea na michango ya ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji hicho hadi hapo serikali itakapomwajibisha msimamizi wa ujenzi huo anaetuhumiwa kufanya ubadhirifu wa fedha zaidi ya shilingi milioni mbili zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo.

Mtendaji wa kijiji hicho Bwana REMDI KANOKA amesema wameshatoa malalamiko yao mara kadhaa kwa watendaji wa serikali juu ya ubadhirifu huo lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya msimamizi huyo zaidi ya kuhamishiwa katika kituo kingine huku wakazi hao wakiendelea kupata adha ya matibabu katika jengo lililoharibika.


Akizungumzia juu ya ubadhirifu huo Mganga Mkuu wa Wilaya ya NKASI DK GWAMAKE MWALULAMBO amekiri kupokea taarifa hizo kutoka katika kijiji hicho ambapo ameshindwa kuthibitisha kama msimamizi huyo amerudisha fedha hizo au lah. PICHA KWA HISANI YA MJENGWA!

No comments:

Post a Comment