Tuesday, August 30, 2011

WAKAZI DAR WALALAMIKIA UKOSEFU WA LUKU KWA SIKU NNE!

Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es salaam wamelilalamikia Shirika la Umeme nchini TANESCO kutokana na uwepo wa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Luku lililodumu siku ya nne sasa.

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wakazi hao wameelekeza tuhuma zao kwa watendaji wakuu wa shirika hilo kwa kushindwa kulishughulikia tatizo lililopo hali inayofanya wananchi waendelee kuishi katika hali ngumu ya kukosa umeme hasa katika kipindi hiki cha sikukuu.


Kituo hiki kilipofika Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam kupata ufafanuzi kuhusiana na suala hilo mmoja ya wafanyakazi amesema watendaji wakuu ambao ndio wasemaje walikuwa nje ya ofisi kushughulikia tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment