Jeshi la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limejipanga vyema kukabiliana na vitendo vya uvunjifu wa sheria na kanuni za barabarani vinavyofanywa na madereva wazembe katika msimu huu wa sikukuu ya Eid EL Fitri.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani SACP MOHAMMED MPINGA, amesema kikosi chake kitakuwa katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha sikukuu inasherehekewa kwa amani na utulivu kwa kudhibiti makosa mbalimbali ya barabarani.
Sanjari na hatua hiyo Kamanda MPINGA amewaomba madereva kote nchini kutembea na leseni zao kwani jeshi hilo litaendesha msako kuwabaini wote wanaoendesha magari bila kuwa na leseni zinazostahili kulingana na vyombo vya moto wanavyovitumia.
No comments:
Post a Comment