Tuesday, August 30, 2011

WAASI LIBYA WATAKA MKE WA MUAMMAR GADDAFI AREJESHWE LIBYA

Waasi nchini Libya wanatafuta namna ya kurejeshwa kwa mke wa MUAMMAR GADDAFI na watoto wake watatu nchini humo, wakati ambapo wanaendelea na jitihada za kumsaka kiongozi huyo. Akizungumza baada ya Algeria kutangaza kuwa mkewe GADDAFI, SAFIYA pamoja na watoto wawili wa kiume, binti yake na watoto wao wamevuka mpaka na kuingia nchini humo, Msemaji wa waasi, MAHMUD SHAMMAM alisema kwamba wangependa watu wote hao warejeshwe.

Mpaka sasa, Algeria haijalitambua Baraza la Waasi na imekuwa na msimamo wa kutoegemea upande wowote katika mgogoro wa Libya, hata hivyo miongoni mwa waasi wamekuwa wakiituhumu nchi hiyo kuunga mkono utawala wa GADDAFI. Katika taarifa iliyotangazwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi hiyo, imetaja majina ya watoto wa GADDAFI ambao wamevuka mpaka Libya na kuingia Algeria kuwa ni AISHA, HANIBAR na MOHAMMED.


Miongoni wa waliotajwa kupata taarifa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa BAN KI-MOON, Baraza la Usalama la Umoja huo pamoja na Kiongozi namba mbili wa waasi wa MAHMUD JIBRIL. Nalo Shirika la Habari la ANSA, likinukuu vyanzo vya kuaminika vya kidiplomasia vya Libya vikisema GADDAFI GADDAFI na wanawe SAADI pamoja na SEIF AL-ISLAM wamejificha katika mji unaoitwa BANI WALID, uliopo kusini mwa Tripoli.

No comments:

Post a Comment