Tuesday, August 30, 2011

WAZAZI JIJINI WAKIRI KUCHANGIA WATOTO KUTOROKA MAJUMBANI!

Kutokana na idadi ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kuongezeka nchini, baadhi ya wazazi Jijini Dar es salaam wamekiri kuchangia hali hiyo kutokana na vitendo vya kikatili ambavyo wamekuwa wakifanya dhidi yao.

Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti wazazi hao wamesema kuwa, mbali na vitendo hivyo pia kutofautiana na kutengana kwa wazazi katika familia ni miongoni mwa sababu ya watoto kuendelea kutoroka majumbani mwao.

Kwa upande wao baadhi ya watoto waishio katika mazingira magumu, Jijini Dar es salaam wamekiri kufanyiwa vitendo vya kikatili na wazazi wao ikiwa ni pamoja na kuwapiga wakiwashinikiza kwenda mitaani kutafuta fedha za kujikimu kimaisha.

No comments:

Post a Comment