Friday, July 8, 2011

ZAIDI YA ASILIMIA 70 YA WANAWAKE WALIO KWENYE NDOA SINGIDA WAMEBAKWA!

ZAIDI ya asilimia 70 ya wanawake walioolewa katika halmashauri ya wilaya ya Singida, wamewahi kufanyiwa vitendo vya ubakaji na waume zao, wakiwa kwenye ndoa zao.

Hayo yamebainishwa jana na mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya hiyo Dk.Dismas Nyagusa, kwenye warsha iliyondaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ‘Medicos del Mundo’, kutoa matokeo ya utafiti wa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia,wilayani humo.


Imeelezwa kuwa hatua hiyo inachangia mimba zisizo tarajiwa, ongezeko la vitendo vya utoaji mimba, hata wakati mwingine familia kupata watoto wengi wanaokosa mahitaji muhimu,katika kaya.


Amesema kuwa, pamoja na vitendo vingine vingi vya unyanyasaji ikiwemo ukeketaji na kupigwa kwa wanawake,pia utafiti huo umeonyesha ubakaji kwenye ndoa ni tatizo sugu linalowakabili wanawake wengi, wilayani humo.

Kwa upande wake mratibu miradi wa shirika hilo Bibi.Victoria Mwivano amesema,lengo la utafiti huo ni kufahamu kwa kina ukubwa wa tatizo la unyanyasaji kijinsia, ili kwa kushirikiana na wadau wake, iwekwe mikakati madhubuti kukabiliana nalo.

No comments:

Post a Comment