Friday, July 8, 2011

WAZAZI WA KABILA LA GOGO WASEMA MILA NA DESTURI KWA WATOTO WAO ZINAWAJENGA KIMAADILI!

Baadhi ya wazazi kutoka kabila la la wagogo wilayani bahi mkoa wa Dodoma wamesema mila na desturi wanazowafanyia watoto wao wa kiume wakati wa jando zinalengo la kuwajenga watoto wao kimaadili kulingana na taratibu za kabila hilo.

Mmoja wa mzazi wa vijana hao BWANA METHEW STEVEN amesema kwa sasa mila hizo hufanyika wakati shule zinapokuwa zimefungwa, ili ratiba za masomo zisiingiliane na taratibu hizo.


Amesema baada ya vijana hao kupona wanalazimika kukaa klatika makambi maalum kwa zaidi ya wiki tatukupata mafunzo maalum kama kutunza mifugo na kufanya kazi za kijasiri ikiwa ni pamoja na kuwinda na pia kukutanishwa na wazee wa jadi kupata mafunzo ya kiulinzi pamoja na usalama wao.

No comments:

Post a Comment