Friday, July 8, 2011

PINDA AWATAKA WAWEKEZAJI KUIGEUKIA SEKTA YA MIUNDOMBINU YA GESI!

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema umefika wakati kwa wawekezaji wa kimataifa kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika miundombinu ya kusafirisha gesi asilia kama njia mojawapo ya kusaidia kukuza uchumi wa Tanzania.

Amesema kupatikana kwa gesi nyingi katika ukanda wa pwani ya kusini mwa Tanzania kunatoa fursa ya wawekezaji kuanza kufikiria ujenzi wa mabomba ya gesi ili bidhaa hiyo iweze kutumika viwandani, kuendesha mitambo pamoja na viwanda.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu kwa vyombo vya habari, imesema waziri Pinda Ametoa kauli hiyo leo mchana kwenye hoteli ya Samsung mjini Geoje, wakati akiwahutubia wageni maalumu kutoka makampuni mbalimbali ya wawekezaji walioalikwa kuhudhuria uzinduzi wa meli ya uchimbaji mafuta iitwayo Poisedon katika bandari ya Geoje, iliyoko kusini mashariki mwa Seoul, mji mkuu wa Korea Kusini.


Kwa upande wa Petrobras, kampuni ya Brazil ambayo itaendesha utafiti nchini Tanzania, Waziri Mkuu alisema ana matumaini na kampuni hiyo kama mbia makini kutokana na historia ambayo imejiwekea duniani tangu mwaka 1952 ilipoanzishwa.

No comments:

Post a Comment