Friday, July 8, 2011

WAKALA WA MAJENGO YASEMA UKARABATI WA MAHAKAMA UTAKUWA ENDELEVU!

Wakala wa Ujenzi nchini (TBA), umesema ujenzi na ukarabati wa mahakama nchini kote utakuwa endelevu ukihusisha pia mahakama za mwanzo, Wilaya pamoja na zile za rufaa.

Akizungumza wakati wa maonyesho ya kimataifa ya Sabasaba, Jijini Dar es salaam, Msanifu wa Majengo Mwandamizi ( TBA), DEOGRATIUS CHUBWA, amesema ukarabati huo ambao ni miongoni mwa utekelezaji wa agizo la Rais JAKAYA KIKWETE, utahusisha mazingira kwa ujumla ya mahakama zote nchini.


Katika hatua nyingine Wakala huo umedai kuwa umeshaanza kutatua tatizo la uhaba wa makazi kwa baadhi ya viongozi wa Serikali nchini wakiwemo Mawaziri.

No comments:

Post a Comment