Saturday, July 16, 2011

KAMBI YA REDDS MISS ILALA YAANZA PARADISE CITY HOTEL!

Warembo 20 wa Redds Miss Ilala 2011 wameanza kambi yao ya mazoezi jana kwenye hoteli ya kitalii ya nyota nne iliyoko katikakati ya jiji la Dar es salaam. Paradise city Hotel iko kwenye jingo la ghorofa ishirini na moja la Benjamin William Mkapa towers lililoko posta mpya.
Warembo wako chini Regina Mromi kama mkuu wa kambi ambaye aliwahi kushiriki mashindano ya Miss Tanzania akitokea mkoa wa singida na pia aliwahi kuwa Miss Ukonga na kushiriki Miss Ilala mwaka 2003. Mwalimu wa catwalk ni Anneth Kagua aliyewahi kushinda nafasi ya pili ya Miss East Africa na Miss Tabata 2008 na mwalimu wa dansi ni wanne star. Matron wa Warembo ni Bahati Chando ambaye ni Redds Miss Ilala anaye maliza muda wake.

Kesho jumamosi, Hotel ya Paradise City imeandaa sherehe za kuwakaribisha warembo katika hotel yao ambapo kutakuwepo chakula cha usiku na ku dance. Watu wanakaribishwa katika hafla hiyo ambapo hoteli imeweka kiingilio cha SHs 20,000/= kwa kila atakayeingia kwenye hafla hiyo itakayotumbizwa na bendi ya bora bora ya hapa Dar. Baada ya sherehe hiyo warembo wa Ilala wataondoka kwenda kwenye shindano la Miss temeke.


Jumamosi asubuhi saa nne, mrembo wa Tanzania ambaye alitokea Ilala atatembelea kambi kwenye hotel hiyo na kuendesha mafunzo ya ya nadhalia kwa warembo. Hoyce atawafundisha warembo namna ya kujielewa kama warembo, kujiheshima kama wasichana na jinsi kwenye shughuli mbali mbali za kijamii na kuishi vyema kama wazelendo na watu wanaotegemewa na jamii. Tunategemea pia kuwa Hoyce atawafunda warembo wa Ilala kwa ajili ya kinyanganyiro cha Vodacom Miss Tanzania.


Shindano la Redds Miss Ilala 2011, limedhaminiwa na Tanzania Breweries limited kupitia kinywaji chao cha Redds Original kama wadhamini wakuu na Vodacom Tanzania kama wadhamini washiriki. Wadhamini wengine ni Paradise city Hotel, Paris Pub, Maisha Club, Tanzania standard newspapers, Syscorp Group, Fabak fashion, Michuzi Blogspot, Uchumi Supermarket, TV Sibuka na Channel ten.

No comments:

Post a Comment