Saturday, July 16, 2011

RAIS KIKWETE NA MAKAMU WA RAIS WAHUDHURIA NDOA YA YUSUPH KIKWETE BAGAMOYO!

Rais jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt Mohammed Gharib Bilal, wakiongozana katika Uwanja vya Ikulu Ndogo Bagamoyo wakati walipofika kuhudhuria sherehe ya ndoa ya mdogo wake na rais Kikwete, Yusuph Kikwete, iliyofungwa leo mchana katika uwanja huo na kuhudhuriwa na mbalimbali pamoja na wake za viongozi.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Bilala, wakiwa katika meza kuu kwenye Sherehe hiyo iliyofanyika Bagamoyo leo.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa kwenye picha ya pamoja na maharusi wao
Mama Salma Kikwete (kushoto) akiwa na Mama Zakhia Bilal (katikati) na Mama Asha Bilal, wakati wakiwa katika sherehe hiyo ya ndoa ya mdogo wake na Rais Jakaya Kikwete, Yusuph Kikwete leo mjini Bagamoyo.
Bwana harusi, Yusuph Kikwete akiongozana na wapambe wake wakati wakiingia katika uwanja huo kwa ajili ya kufunga ndoa.
                                      Bwana Harusi, Yusuph, akifungishwa ndoa na Sheikh.
Bwana Harusi Yusuph na waumini wa dini ya Kiislamu wakiomba dua baada ya tendo la kufungishwa ndoa.

No comments:

Post a Comment