Monday, July 11, 2011

POLISI JIJINI YAWATAKA WANANCHI KUWA MAKINI WANAPOSAFIRISHA FEDHA!

                                                                 SACP Suleiman Kova.
Jeshi la polisi kanda maalum ya DSM limewataka wananchi, taasisi pamoja na makampuni mbalimbali kuwa makini wanapokuwa wakisafirisha fedha nyingi bila ya kuwa na ulinzi wa kutosha kutokana na kuibuka kwa Vitendo vya Uporaji hapa jijini.

Tahadhari hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM ABDUL NINA wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari.


Kwa upande wake Mkuu wa upelezi wa makosa ya jinai wa kanda hiyo AHMED MSANGI ameyataka makampuni, taasisi kuanza kutumia njia ya electroniki ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.

No comments:

Post a Comment