Thursday, June 30, 2011

ZITTO KABWE AKEMEA WABUNGE KUTOELEZA WAZIWAZI MASUALA AMBAYO WANANCHI HAWAYATAKI!

JENGO LA BUNGE 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini ZITTO KABWE amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kuogopa kueleza waziwazi masuala ambayo wananchi hawayataki kwa kuwa yanachangia jamii kutolielewa bunge.
Akichangia Makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni mjini Dodoma kuhusiana na ongezeko la bei ya mafuta ya taa mheshimiwa KABWE amesema kutokana na hali hiyo serikali itoe agizo kwamba ushuru wote ulioongezeka kwenye bidhaa hiyo upelekwe kwenye uzalishaji umeme vijijini.
Katika hatua nyingine mbunge huyo ametoa rai kwa serikali kuacha kuyavutia makampuni yanayofanya utafiti wa mafuta nchini kwani Tanzania tayari ina kampuni nyingi zinazofanya kazi hiyo na kubaini uwepo wa kiwango kikubwa cha mafuta na gesi.

No comments:

Post a Comment