Friday, July 1, 2011

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA IPASAVYO MFUKO WA AFYA YA JAMII!

Wananchi wametakiwa kujenga tabia ya kutumia kikamilifu mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwa lengo la kukabiliana na changamoto mbali mbali zilizopo katika sekta ya afya sambamba na kuweka mikakati ya kusaidia kupunguza gharama za matibabu. Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini,SILVESTRY KOKA, amesema kwamba ana imani kuwa kujiunga katika mfuko huo ni moja ya njia mbadala ya kupunguza kero za matibabu pamoja na gharama zake.


Aidha KOKA ,amebainisha kuwa ,serikali kupitia Halmashauri zake ina mpango kabambe wa kuhakikisha kila kata inafikiwa na huduma ya afya na kwamba atashirikiana na wananchi hao katika kufikia malengo ya kusogeza huduma za afya jirani na makazi yao. Wakati mchakato wa kujenga zahanati hiyo ukiendelea Mbunge huyo amewataka wananchi hao kujiunga na mfuko huo wenye gharama ya Sh,5000 kwa mwaka ambapo watu zaidi ya 10 wanakuwa wakitibiwa kupitia gharama hizo.

No comments:

Post a Comment