Thursday, June 30, 2011

MBUNGE LEMBELI AHOJI UHALALI WA SERIKALI KUIGAWA KAHAMA KWA BARRICK GOLD MINE!

Mbunge wa Kahama kupitia CCM, JAMES LEMBELI amehoji uhalali wa serikali kuigawa Wilaya yote ya Kahama kwa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Mine jambo linalochangia wananchi kushindwa kujiletea maendeleo.

Akichangia Makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni mjini Dodoma LEMBELI amesema hali ilivyo sasa mtu anapochimba mawe kwa ajili ya ujenzi watendaji wa sekta ya madini na walinzi wa Kampuni ya Barick humkamata na kumfungulia mashitaka kwa kuchimba madini bila kibali.
Kutokana na suala hilo JAMES LEMBELI amemuomba Waziri wa Nishati na Madini WILLIAM NGELEJA kufikiria mustakabali wake wa baadae mara atakapotoka kwenye wadhifa huo.

No comments:

Post a Comment