Tuesday, June 14, 2011

WAKAZI DSM WATOA MAONI YAO KUHUSIANA NA POSHO ZA WABUNGE!

Wakazi Jijini Dar es salaam, wametoa maoni yao kufuatia mvutano unaoendelea Bungeni juu ya hoja ya kufutwa kwa posho zisizonatija za Wabunge na Watumishi wengine serikalini.

Wakizungumza na kituo hiki wakazi hao, wameonekana kutofautia kufuatia baadhi yao kuunga mkono hoja hiyo na wengine kupinga kwa madai kuwa Wabunge wanakabiliwa na majukumu mengi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maendeleo yanadhihilika kwenye majimbo yao.
Hayo yamekuja kufuatia baadhi ya Wabunge kutoka Vyama vya upinzani nchini wakiwemo wa CHADEMA pamoja na NCCR- Magezuzi, kutaka Posho hizo zifutwe.

No comments:

Post a Comment