Tuesday, June 14, 2011

JAMII YATAKIWA KUTOWABAGUA WATOTO WA MITAANI!


Serikali imewakumbusha wananchi pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kuwa watoto ni taifa la leo na kesho hivyo wanapaswa kuendelezwa ,kulindwa kushirikishwa na kutobaguliwa.

Ujumbe huo umetolewa katika taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na katibu mkuu wa wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto Bwana KIJAKAZI MTENGWA wakati Taifa linapoelekea kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika June 16 mwaka huu huku kauli mbiu ikisema Tuungane kwa pamoja kuchukua hatua za haraka kushughulikia tatizo la watoto wanaoishi mitaani.


Hata hivyo wakazi wa jiji la DSM wamedai kuwa tatizo la ongezeko la watoto wanaoishi mitaani linaendelea kuwa sugu nchini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya familia nyingi kutokuwa na malezi bora kwa watoto na tabia iliyoanza kujitokeza siku hizi ya ndugu kuacha kuleleana watoto

Aidha kwa mujibu wa wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto imesema kwa mwaka huu hapatakuwepo na maadhimisho kitaifa bali kila mkoa utapata fursa ya kupanga namna ya kuadhimisha siku hiyo.

No comments:

Post a Comment