Thursday, June 23, 2011

UUZWAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI WASABABISHA UHABA WA NYUMBA ZA WATUMISHI!

Wakala wa Majengo nchini umesema ukosefu wa makazi kwa baadhi ya Watumishi wa Serikali umesababishwa na mchakato wa uuzwaji wa baadhi ya nyumba za Serikali.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanaliyomalizika jana jijini DSM, Msanifu wa Majengo Mwandamizi, DEOGRATIUS CHUBWA, amesema wamejipanga kutatua tatizo la ukosefu wa makazi kwa Watumishi hao kupitia mkakati wa ujenzi wa makazi kwa muda mfupi.
Katika hatua nyingine, Afisa uhusiano wa Idara ya Majengo, SEGOLENA FRANCIS, amesema Idara hiyo imeazimia kununua viwanja maeneo mbalimbali nchini, ili kuongeza makazi ya kutosha kwa watumishi Serikalini.

No comments:

Post a Comment