Thursday, June 23, 2011

WAKALA WA HIFADHI YA CHAKULA (NFRA) YAONGEZA UWEZO WA KUNUNUA HIFADHI YA CHAKULA HADI TANI 140,000!

Serikali kupitia Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) imeongeza uwezo wake wa kununua mahindi kutoka kwa wakulima kuanzia tani 140,000 hadi tani 350,000 za mahindi kwa mwaka.

Hayo yamebainishwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Razaro Nyalandu wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbozi Mashariki kupitia CCM Weston Zambi ambaye alitaka kujua lini Serikali itawahakikishia wananchi wa Wilaya ya Mbozi soko la uhakika kutokana na wananchi hao kuwa ni wakulima hodari lakini hawana sehemu ya kuuzia mazao yao.
Akijibu swali hilo Waziri Nyalandu amesema Serikali imeanzisha bodi ya Mazao mchanganyiko ambayo inatarajia kuanza kununua mahindi katika msimu wa mwaka 2011/2012.

No comments:

Post a Comment