Wednesday, June 15, 2011

KASI YA UKOPAJI WA SERIKALI SIO ENDELEVU NA NI MZIGO KWA KIZAZI KIJACHO: UPINZANI BUNGENI!

Kambi ya Upinzani Bungeni imesema ingawa mataifa yote yanayoendelea duniani hukopa fedha kutoka kwa wahisani lakini kasi ya ukopaji wa Serikali sio endelevu na ni mzigo mkubwa kwa kizazi kijacho kutokana na asilimia 50 ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2011/2012 itagharamiwa na kodi na asilimia 30 kutegea fedha za mikopo.

Akisoma mapendekezo ya Bajeti ya Kambi ya Upinzani Bungeni , Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo Wizara ya Fedha ZITTO KABWE amesema asilimia 30 ya gharama za leo zitabebwa na kizazi kijacho hivyo kutokana na hoja hiyo kambi hiyo inapendekeza ufanyike uchunguzi maalum ili kubaini jinsi madeni haya yatakavyotumika.
Katika hatua nyingine amesema serikali haina budi kudhibiti matumizi yake kwani kwa mwaka 2008/2009 ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali ilionesha kwamba takribani asilimia 25 ya bajeti yote zilitumika na mafisadi.

           KAMBI YA UPINZANI BUNGENI -MAPATO YA SERIKALI HADI TRILLIONI 14/-!
Kambi ya upinzani Bungeni imesoma mapendekezo ya Bajeti Mbadala ya kambi ya Upinzani kwa mwaka 2011/2012 huku ikitaja vipaumbele kadhaa ikiwemo kuongeza mapato ya serikali kufikia trillioni 14 kutoka 13 za serikali, kuondoa kukopa mikopo yak kibiashara na kuweka fedha za kutosha kwenye miradi ya umeme na gesi.
Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo Wizara ya Fedha ZITTO KABWE amesema bajeti hiyo pia imependekeza kwamba vivutio vinavyotolewa na Kituo cha Uwekezaji cha Taifa TIC vipigwe marufuku kutolewa msahama wowote wa kodi wa bidhaa zinazozalishwa nchini ili kulinda viwanda vya ndani.
Katika hatua nyingine amesema kuna haja taifa kuhakikisha taifa linakusanya mapato ya kutosha katika sekta ya madini kwa kuangalia upya mfumo wa utoaji mikopo kwa wawekezaji ili kusaidia kuwaletea wananchi maendeleo.

              SERIKALI IPUNGUZE USHURU WA BIDHAA ZA MAFUTA KWA ASILIMIA 40!
Serikali imeombwa kupunguza ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa za mafuta kwa asilimia arobaini na tozo zingine zote zinazohusiana na bidhaa hiyo kwa asilimia arobaini ikiwemo kufuta kabisa misamaha ya kodi kwenye mafuta kwa kampuni za madini na za ujenzi
Akisoma mapendekezo ya Bajeti ya Kambi ya Upinzani Bungeni , Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo Wizara ya Fedha ZITTO KABWE amesema takwimu zinaonesha kwamba misamaha hiyo imethibitika kuchangia upotevu mkubwa wa fedha za umma na kwamba mafuta mengi yanayoingia kwa njia hiyo huuzwa rejareja.
Wakati huo huo KABWE amesema kambi ya upinzani inapinga serikali kuondoa misamaha ya sasa ya kodi kwa kampuni za utafutaji mafuta nchini kwani mkataba wao unaonesha watarejeshewa mafuta yao mara yatakapopatikana.

No comments:

Post a Comment