Wednesday, May 11, 2011

PINDA AWATAKA VIONGOZI WA AU KUHIMIZA USINDIKAJI WA MAZAO!

                                                      Waziri mkuu MIZENGO PINDA

Waziri mkuu MIZENGO PINDA amewataka viongozi wa umoja wa nchi za Afrika AU ikiwemo Tanzania kuhimiza uwepo wa vyombo maalum vya kusindikia mazao na bidhaa mbalimbali katika nchi zao kwa ajili ya kuendeleza viwanda vitakavyoleta chachu za kimaendeleo baina ya nchi hizo.



Akifungua mkutano mkuu wa maeneo huru ya uwekezaji Afrika AFZA hapo jana ,Waziri PINDA amesema endapo viwanda vikiongezeka katika nchi za afrika kutatoa mianya kwa wananchi kupata ajira ambayo itawawezesha kupambana na umasikini huku akiitaka Tanzania nayo kuboresha sekta zake za maji na umeme ili kuvutia zaidi wawekezaji.

Nae Mkurugenzi mkuu wa maeneo huru ya uwekezaji nchini EPZA Bwana ADELHEM MERU amesema pamoja na masuala mbalimbali kujadiliwa katika mkutano huo pia umelenga kusaidia wawekezaji wa ndani kujenga mbinu ya kuunda ukanda wa uwekezaji afrika ili kuwawezesha kuwa wawezeshaji mkuu katika kuhakikisha malengo ya maendeleo ya millennia yanafanikiwa.

Kauli mbiu ya mkutano huo unaojumuisha nchi 21 kutoka mataifa mbalimbali duniani ambao kwa mara ya kwanza ulifanyika ABUJA nchini NIGERIA mnamo mwaka 2008, ni jukumu la maeneo huru ya uwekezaji katika kufikia malengo.

No comments:

Post a Comment