Wednesday, May 11, 2011

HALI YA UCHAFU YAWATISHIA WAFANYABIASHARA SOKO LA TANDALE!

Wafanyabiashara wa soko la Tandale, Jijini Dar es salaam wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kufuatia kuwepo kwa miundombinu mibovu inayosababisha usumbufu kwa wateja kushindwa kujipatia mahitaji ya kila siku katika soko hilo.


                                Lori la Mahindi likishusha bidhaa hiyo sokoni Tandale
Makamu Mwenyekiti wa soko la Tandale,Juma Janga amesema miundombinu ya soko la Tandale, imeharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa, huku watumiaji wa soko hilo wakishindwa kufika kwa urahisi kujipatia mahitaji kutoka sokoni hapo.
                                           Hali ya uchafu inavyoonekana sokoni hapo
Kwa upande wa wateja wamesema hatua hiyo imekuwa kero na usumbufu kwao na kuilalamikia serikali kushindwa kuwajibika ipasavyo kutokana na hali ilivyo kuwa kwa muda mrefu bila kutatuliwa.
Hii ndio halisi inavyoonekana kama ilivyokutwa na Mwanaeastafrica leo hii
Kutokana na tope jingi katika soko la Tandale, wadau baada ya kumaliza kazi wanapata huduma ya kuoshwa miguu kwa gharama ya shilingi 100 kwa kichwa....Tembea uone!

No comments:

Post a Comment