Sunday, May 15, 2011

MSAMA PROMOTION YATOA MSAADA MILIONI 4/- KWA WAJANE!

Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Pasaka Alex Msama (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi fedha zilizokusanywa kupitia tamasha hilo kwa ajili ya wajane na watoto yatima. Kushoto ni mjumbe wa kamati hiyo Jimmy Charles na kulia ni Afisa Habari wa kamati hiyo Denis Fussi.
Msama Promotions yatoa mil 4 kwa wajane

Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE Msama Promotions waandaaji wa Tamasha kubwa la Pasaka wamekamilisha ahadi yake ya kuwasaidi wanawake wajane fedha za mitaji ya biashara kwa kuwakabidhi wajane 24 fedha taslimu sh. 150,000 kila mmoja.

Akikabidhi fedha hizo, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, alisema kwamba sasa ametimiza ahadi aliyoitoa wakati wa maandalizi ya tamasha la Pasaka lililofanyika Aprili 24 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee huku mgeni rasmi akiwa ni rais wa jamhuri wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Aidha Msama alisema kwamba fedha hizo zimepatikana kutokana na mauzo ya albamu ya Haleluya Colletion Vol 5 ambayo ilizinduliwa katika Tamasha la Pasaka.

“Leo tunatimiza ahadi yetu ya kuwapatia wanawake wajane fedha za mitaji ya biashara kama ambavyo tuliahidi wakati wa maandalizi ya tamasha la Pasaka,” alisema Msama
Wanawake hao wajane waliokabidhiwa fedha hizo za mitaji wametoka katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambapo jumla ya shilingi milioni 4 zimetumika.

Pia fedha fedha zilizopatikana kwenye Tamasha hilo zitatumika kuwasaidia kuwasomesha watoto yatima. Msama Promotions tayari imeshatoa msada wa shilingi milioni tatu kwa waathirika wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Picha za juu Alex Msama akikabidhi fedha hizo kwa wajane.
Baadhi ya wajane waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa fedha na Kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha la Pasaka wakimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni hiyo Alex Msama.

No comments:

Post a Comment