Sunday, May 15, 2011

BREEEEEEAKING NEWS....MCHINA AZAMA KUNDUCHI BEACH HOTEL!

Hotel ya kimataifa ya Kunduchi Beach Hotel
                                                     Ufukwe kwa Hotel ya Kunduchi Beach
Raia mmoja wa kigeni mwenye asili ya China anasadika kufa baada ya kuzama na kupotea wakati akigelea kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Taarifa zilizoifikia sasa hivi blog hii ya jamii zinaeleza kwamba Wachina hao wawili walikuwa wakiogelea kwenye ufukwe wa hoteli hiyo kabla ya mmoja kuzama na kutokomea kwenye kina cha maji cha ufukwe huo.

Habari zaidi zinasema kwamba mmoja ya Wachina hao ameokolewa na kupatiwa huduma ya kwanza wakati juhudi za kumtafuta aliyezama kwenye maji zikiendelea.

Taarifa zisizo rasmi zinasema baadhi ya waandishi wa habari walio katika eneo hilo kusubiri kufunguliwa kwa mkutano wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ALAT wanazuiliwa kwenda eneo la tukio na uongozi wa hoteli hiyo.

Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea blog hii ya jamii yenye muonekano mpya kwa uelewa!

No comments:

Post a Comment