Tuesday, May 17, 2011

MAGUFULI ATAKA WAHANDISI WAZALENDO KUFANYA KAZI KWA MOYO!

Serikali imewataka wahandisi wazalendo kufanya kazi kama wachungaji ili kulifanya taifa kuwa na miundondominu inayokidhi viwango vya kimataifa, tofauti na hivi sasa ambapo wengi wao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa maslahi yao Binafsi.


Akizungumza jijini DSM katika Ufunguzi wa mkutano wa Bodi ya Usajiliwa wa wakandarasi ERB, Waziri wa Ujenzi Dakta JOHN MAGHUFULI amesema Sababu inayochangia wakandarasi wa Kigeni kupatiwa tenda za Kazi kunatokana na wakandarasi wazalendo kushindwa kusimamia kazi za ujenzi ipasavyo licha ya serikali kutoa kipaumbele kwa wazawa.


Mkutano huo wa siku moja uliandaliwa na Bodi ya Usajili Wahandisi ili kuzungumzia utoaji wa leseni mpya za wahandisi wanaofanya kazi hiyo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment