Tuesday, May 17, 2011

BAADHI YA WAKAZI SHINYANGA WATUMIA MAJIVU KUJIKINGA NA UKIMWI!

Kumekuwepo na taarifa kwamba baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wamekuwa wakikoroga majivu na kuyanywa kabla ya kujamiiana kwa lengo la kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.


Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Shinyanga Dakta Charles Mashenene wakati wa mahojiano na kituo hiki amekiri kuwepo kwa imani hiyo potofu hasa kwa wakazi wa kata ya Ndala mkoani humo na hivyo kuwataka waachane na imani potofu na badala yake wafuate kile ambacho wataalamu wa afya wanaelekeza juu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU.


Katika hali isiyokuwa ya kawaida mmoja wa wakazi wa kata hiyo ya ndala Bi Martha Chilindi, licha ya kukiri kuwepo kwa imani hiyo potofu lakini anaweka wazi namna ambavyo wanawake hasa wanafunzi wa kata hiyo kuyatumia majivu kwa kutoa mimba, huku wale wanaonyonyesha wakiyatumia kama kirutubisho cha maziwa kwa mtoto.


Jitihada za kuwapata wataalamu wa afya ili kulizungumzia suala hili zinaendelea.

No comments:

Post a Comment