Tuesday, May 17, 2011

HABARI KUTOKA VYANZO MBALIMBALI VYA HABARI JIONI HII!

             MGAO WA UMEME MIKOA 12 KUWA KAA LA MOTO KWA WATANZANIA!
                                                                         Badra Masoud
                                                            Mitambo ya Umeme Kihansi
WANANCHI wa mikoa 12 wataendelea kupata machungu ya mgao wa umeme, baada ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kutangaza tena ratiba ya mgao huo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo asubuhi kwenye vyombo habari kutoka kitengo cha mawasiliano Makao Makuu TANESCO, na kusainiwa na Ofisa Uhusiano, Badra Masoud.

Imeeleza kuwa, mgawo huo utahusisha Mkoa wa Dodoma, Morogoro, Mara, Tabora, Pwani, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Iringa, Mbeya, Manyara na Dar es Salaam katika wilaya zote za Temeke, Ilala na Kinondoni.

Taarifa hiyo imesema kuwa, umeme huo utaanza kukatika saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni, ambapo katika maeneo mengine, utakatika kuanzia saa 12 jioni na kurejea saa 5, usiku. Hata hivyo, taarifa hiyo imesema kuwa, maeneo mengine mgawo utakuwa ukianzia saa 10 jioni hadi saa 5 usiku, wakati maeneo mengine yatakuwa giza kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.

                     DK HARRISON MWAKYEMBE AJIBU MAPIGO YA MPENDAZOE!
WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kikiendelea na mashambulizi dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuwaanika hadharani wanachama wake wanaodaiwa kuanzisha Chama Cha Jamii (CCJ), Mbunge wa


Kyela, Harrison Mwakyembe, ameibuka na kusema kuwa, CHADEMA wanaingilia kazi za msajili wa vyama vya siasa, John Tendwa.


Akizungumza jijini leo, Mwakyembe amesema kuwa, hana cha kueleza zaidi, ila anayetaka kujua ukweli wa chama hicho, aende kwa Tendwa kwani ndiye anayefahamu ukweli wa jambo hilo ikiwa ni pamoja na waanzilishi wa chama hicho.


Ameongeza kuwa, mwanachama wa CHADEMA, Fred Mpendazoe ameyumba kisiasa na ndiyo maana ameanza kutoa taarifa ambazo hazina uthibitisho kamili, lengo lake likiwa ni kuwachafua watu majina yao.


"Mimi sina la zaidi, lakini ninachoweza kusema, CHADEMA wasimwingilie msajili, kwani yeye ndiye anayejua uhalali na waanzilishi wa chama hicho, hivyo anayetaka ukweli zaidi aende huko akathibitishe hilo," amesema Mwakyembe. Hata hivyo, Mwakyembe aliahidi kulitolea maelezo zaidi suala hilo baadaye leo.


Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye, amesema kuwa yupo tayari kuwajibika kwa lolote, endapo atabainika aliisaidia CCJ kwa namna moja ama nyingine. Amesema kuwa, imefika wakati kwa CHADEMA kufanyakazi halali na kuacha kupika majungu ambayo hatima yake ni kuleta machafuko ya kisiasa ambayo yanaweza kusababisha umwagikaji damu.


Vyombo mbalimbali vya habari, leo viliripoti taarifa iliyotolewa na CHADEMA, ikiwatuhumu Nape, Mwakyemba na Mbunge Samwel Sitta kuwa, ndiyo waanzilishi wa CCJ, kauli ambayo imepingwa vikali na wabunge hao.

Hata hivyo, Dar Leo halikuweza kufanikiwa kumpata Sitta, kwa kuwa simu zake zote za mkononi, zilikuwa zimezimwa.

MTOTO WA AJABU AZALIWA KOROGWE, AFA BAADA YA DAKIKA 10.....ALIKUWA NA PUA YA AJABU NA JICHO MOJA!
Na Mwandishi Wetu, Korogwe

WAKAZI wa Mombo mwishoni mwa wiki walishikwa na butwaa, baada ya kumshuhudia mtoto wa ajabu aliyezaliwa kwa njia ya upasuaji katika kituo cha afya Mombo.

Akizungumza na Dar Leo, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Masanja Mhezi, amesema kuwa, mtoto huyo alizaliwa Mei 10, mwaka huu, ambapo mama yake alikuwa na maumivu makali ya tumbo pamoja na tumbo kuwa kubwa sana.

Amesema kuwa, baada ya kufika muda wa kujifungua, mama huyo alishindwa ndipo daktari wa zamu alipoamua kumfanyia upasuaji na kumzaa mtoto huyo ambaye alikuwa na uzito wa kilo nne. Imedaiwa kuwa, mtoto huyo amezaliwa ana jicho moja, baada tu ya mdomo, katikati pia ana kitu kirefu mithili ya pua cha urefu wa sentimeta nne 4 juu ya jicho moja maumbile.


Ameongeza kuwa, maumbile mengine yote yalikuwa sawa isipokuwa tu, alikuwa na meno manne chini makubwa, aliishi dakika 10 na akafariki dunia.

Amewashauri wanawake waendelee kuhudhuria kliniki pindi tu wanapohisi ni wajawazito, kwani miezi mitatu ya kwanza ni muhimu kwa upimaji wa matatizo mbalimbali yanayoweza kuleta hali kama hiyo, ikiwemo ugonjwa wa kaswende na kuepuka kumeza dawa bila ushauri wa kitabibu.

No comments:

Post a Comment