Monday, May 16, 2011

KIDATO CHA NNE ZANAKI SEKONDARI WAZUIWA KUFANYA MITIHANI KWA KUKOSA SHILINGI 3,000/-

   Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari Zanaki wakiwa nje baada ya kutolewa kwenye mitihani.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha nne Shule ya Sekondari ya Zanaki jijini wameulalamikia uongozi wa shule hiyo kwa kuwatoa nje ya madarasa na kuwazuia kufanya mitihani ya majaribio kwa madai ya kutokulipa michango mbalimbali ikiwemo shilingi 5,000/- ya gharama za ulinzi shuleni hapo.



Wakizungumza na kituo hiki wanafunzi hao wamesema wanashangazwa na kitendo cha Mkuu wa shule hiyo REHEMA TUZO kuwatoa madarasani kwa kushindwa kulipa michango hiyo kinyume na maagizo ya serikali kuwa wanafunzi wasifukuzwe au kusimamishwa shule kw kushindwa kulipa michango mbalimbali.


Mkuu wa shule hiyo alipotakiwa kuzungumzia suala hilo la kuwazuia baadhi ya wanafunzi kufanya mitihani hiyo ya majaribio kwa kushindwa kutoa michango mbalimbali amesema wanafunzi wote waliokuwa nje kwa wakati huo walimaliza vipindi vyao.

No comments:

Post a Comment