Monday, May 16, 2011

HIZI NI HABARI KUTOKA KWA MWANA EASTAFRICA DODOMA LEO!

UDOM WAUNDA TUME KUCHUNGUZA WANAFUNZI WALIOFANYA FUJO!

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma PROF.IDRIS KIKULA amesema uongozi wa chuo hicho umeunda tume kuchunguza wanafunzi wa kitivo cha mawasiliano na Sayansi Angavu IT ambao hivi karibuni walifanya fujo na kusababisha kitivo hicho kufungwa kwa muda usiojulikana.


PROF.KIKULA amesema , matokeo ya Tume hiyo ndio yatakayotoa muongozo wa mwanafunzi anayestahili kurudi chuoni kuendelea na masomo na nani ambaye hastahili kuendelea na msomo chuoni hapo.

Kwa mujibu wa Prof.Kikula amedai kuwa kitendo cha wanafunzi kuandamana mpaka katika ofisi ya waziri Mkuu ni utovu wa Nidhamu lakini pia ni uvunjifu wa amani ya chuo.

Hivi karibuni wanafunzi wa kitivo hicho waligoma na kuandamana hadi katika ofisi ya Waziri Mkuu wakidai kila mmoja kupatiwa kompyuta ambapo wanafunzi 27 walisimamishwa chuo na hatimaye kitivo hicho kufungwa kwa muda usiojulikana kupisha uchunguzi wa tume.

WAKAZI DODOMA WALALAMIKIA WATUMISHI ZAHANATI YA ISANGA KUTOZA PESA WAGONJWA!

Baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma wamelalamikia kitendo cha watumishi wa zahanati ya Isanga iliyopo Manispaa ya Dodoma kutoza pesa kwa watoto walio chini ya miaka mitano kwa ajili ya kuchangia huduma za afya .

Wakizumgumza mjini humo wakazi hao wamesema kinachofanywa na watumishi hao ni kinyume na sera ya Afya ya Taifa inayosema kila mtoto aliye chini ya umri wa miaka mitano anapaswa kutibiwa bure lakini pia ni kuwakosesha watoto haki yao ya msingi.

Aidha wamesema mbali na kutoza pesa kwa watoto wadogo lakini pia watumishi hao wamekuwa na tabia ya kutotoa stakabadhi kwa wagonjwa wote wanaotibiwa katika zahanati hiyo.

Akizungumzia suala hilo Mganga MKuu wa Zahanati hiyo DKT. ALEX BUHIMU amesema kuwa Magereza ni sehemu ya Serikali hivyo watoto hawapaswi kuchangia huduma za afya kama Sera ya Afya ya Taifa inavyosema kuwa mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano anapaswa kutibiwa bure.

No comments:

Post a Comment