SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imepanga kutumia kiasi cha Sh150milioni kwa ajili ya mashindano ya NSSF Media Cup. Mashindano hayo yatafunguliwa rasmi na Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka machi 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Meneja kiongozi wa Idara ya Uhusiano na Huduma za Wateja Eunice Chiume ameeleza kuwa mashindano hayo yatashindaniwa kwa mtindo wa ligi kwa muda wa wiki tatu.
“NSSF imepanga kutumia Sh150milioni kwa ajili ya garama za ununuzi wa vifaa vya michezo pamoja na garama za kuendesha mashindano”alisema Chiume. Akifafanua kuhusu zawadi hizo anasema upande wa mipira ya miguu mshindi wa kwanza atapata fedha taslimu Sh 3.5milioni huku mshindi wa pili akipata Sh2.5milioni na mshindi wa tatu atapata Sh1.5milioni.
“Upande wa netiboli mshindia wa kwanza atapata Sh3milioni, mshindi wa pili Sh2milioni huku mshindi wa tatu akijinyakulia kiasi cha Sh1milioni,pia kutakuwa na wafungaji bora wa mpira wa futiboli na netiboli ambapo kila mmoja atajinyakulia kiasi cha Sh300,000”alisema Chiume.
Timu ya JamboLeo ni moja ya timu zilizowahi kunyakua ubingwa wa mashindano hayo!
No comments:
Post a Comment