Wednesday, March 28, 2012
MICHUZI BLOG YAANZISHA HUDUMA YA KUJIVINJARI BURE KUTOKA UHURUONE!
Muhidini Issa Michuzi akishikiriana na Uhuruone wanawapatia wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya “Wifi hotspots” ambayo itawapa wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya bure ya kutembelea tovuti ya Michuzi. Kwa kupitia mitambo yao ya “Wifi Mesh” iliyopo Dar es Salaam ambayo imeunganishwa na tovuti ya Michuzi,wakazi wa Dar es Salaam wanatangaziwa kwamba wawashe kompyuta zao na kuunganishwa na taarifa za punde bila gharama yoyote.
Akikaririwa katika mahojiano ndugu Issa Michuzi alisema hivi, “Ni mapinduzi ya kweli ambapo Watanzania wanachukua hatua katika kuleta taarifa mbalimbali kwa wananchi katika viwango nafuu. Ninaamini hii itaongeza mawasiliano kwa watu wetu na ni ndoto yangu kwamba tovuti ya Michuzi itakua huru kufika kwa Watanzania wote hivi karibuni”.
Akiwa ofisini Bwana Rajabu Katunda alisema, “Uhuruone imejikita katika kutoa huduma kwa jamii na tumegundua kwamba taarifa za kijamii zinatakiwa kuwafikia wanajamii kwa urahisi. Tovuti nyingi zinatembelewa na Watanzania waliopo nchi za nje kuliko wananchi waliopo nchini na hii siyo haki. Kama nina uwezo kupata taarifa kwenye tovuti ya Michuzi ni jukumu letu kama kampuni kuwawezesha watanzania waliopo nchini pia kupata huduma. Watanzania tunatakiwa kuwa na utamaduni wa kusaidiana na kupeana moyo na hii itasaidia kukuza uchumi wetu sio tu kununua na kuuza bidhaa kutoka nje.
Kwa pamoja Bwana Michuzi na Katunda wamesema huu ni mwanzo tu na wanaamini kwamba hili wazo litafuatwa na wengine. Kwa msisitizo Bwana Michuzi aliongea “Lazima tuonyeshe mfano kwa vitendo sio maneno tu. Tumechukua hatua ya kwanza katika kufanikisha ndoto, wengine wanatakiwa kujiunga kwenye mapinduzi haya na kufanikisha”
Kutembelea tovuti ya Michuzi bila gharama washa Wifi kwenye Ipad, Tablet, Simu au Laptop. Tafuta Michuzi blog Wifi, Unganisha ,fungua browser yako uipendayo mfano Chrome, Internet Explorer, Safari au Firefox na nenda kwa Issa Michuzi.blogspot.com.
Kama hautaona tovuti ya Michuzi Wifi, tafadhali wasiliana na Uhuruone kwa email ifuatayo, issa.michuzi@uhuruone.com au piga simu namba 255779477477 ili uweze kuunganishwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment