Wednesday, March 28, 2012

WAANDISHI WAJIFUNZA SHUGHULI ZA UFUGAJI NYUKI MKOANI SINGIDA!

Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, Bi. Gladness Mkamba akionyeshwa malikia katika mzinga wa nyuki wasiouma na Afisa Nyuki, Bw. Chescho Japhety (aliyeshika bisibisi) huku Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mtanzania, Bw. Kambi Mbwana akishuhudia tukio hilo walipotembelea maeneo ya ufugaji nyuki wilayani Manyoni, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, Bi. Gladness Mkamba akiwaelekeza jinsi ya kutoa asali kwenye sega kwa mwaandishi wa habari wa Gazeti la Mtanzania, Bw. Kambi Mbwana (mwenye fulana) na Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima, Bi. Hellen Ngoromera ikiwa ni sehemu ya ziara iliyolenga kuwajengea uwezo wa kuelimisha jamii kuhusu shughuli za ufugaji nyuki nchini. Katika Ziara hiyo waandishi wa vyombo mbalimbali walipata fursa ya kutembelea vikundi vya ufugaji nyuki katika Wilaya ya Manyoni na Singida mkoani Singida, mwishoni mwa wiki iliyopita.
HAWA SI MABWANA NYUKI NI WAANDISHI WA HABARI WAKIWA WAMEVAA VIFAA MAALUM KWAAJILI YA KURINA ASALI, KUTOKA KUSHOTO NI MWANDISHI WA STAR TV, STEVEN CHEGERE, MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MTANZANIA, BW. KAMBI MBWANA, MWANDISHI WA CHANNEL 10, BW. KIBWANA DACHI, NA MWANDISHI WA GAZETI LA UHURU, BW. MOHAMED ISSA WAKIWA TAYARI KWENDA KUJIFUNZA JINSI YA KURINA ASALI KATIKA ZIARA HIYO.
                          BAADA YA KAZI NGUMU WAANDISHI WALIJIPOZA NA ASALI.

No comments:

Post a Comment