Msafara wa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Arumeru MNashariki Sioi Sumari ukitoka kwenye kambi ya CCM kwenda vijijini kwenye mikutano ya kampeni leo.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha, Nameloki Sokoine akimuombea kura mgombea wa CCM Sioi Sumari kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Kijiji cha Sing'isi, leo.
Aliyekuwa mratibu na mhamasishaji wa kampeni za CHADEMA katika uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki, katika kijiji cha Singisi, Anna Silas akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka baada ya kutangaza kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni ulofanyika leo katika kijiji hicho. Wengine kutoka kulia ni Mwigulu Nchemba na Sioi.
Mwigulu akionyesha kadi za TLP na ya CHADEMA alizokabidhiwa baada ya aliyekuwa Katibu Mwenezi wa TLP Kata ya Seela Sing'isi, Augustine Kyungani na aliyekuwa mratibu wa kampeni za CHADEMA Anna Silas kumkabidhi baada ya kuhamia CCM kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha
Sing'isi leo.
Licha ya jimbo la Arumneru Mashariki kuwa na tatizo la maji katika baadhi ya maeneo, yapo maebeo mengine ambako serikali ya CCM imeweza kuwafikishia wananchi maji ya bomba karibu na makazi yao. Pichani, wanafunzi wakichota maji kwenye bomba la maji safi lililopo kijiji cha Sing'isi leo. (Picha zote na Bashir Nkoromo).
No comments:
Post a Comment