Bi. MARIA KASHONDE
Wanawake wote nchini leo wan adhimisha siku yao ambapo huadhimishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, ifikapo Machi 8, kila mwaka maadhimisho haya hutoa fursa maalum kwa taifa jamii na wanawake katika kupima mafanikio yaliyofikiwa kimaendeleo na kubainisha changamoto zilizojitokeza katika kufikia azma ya ukombozi na maendeleo ya wanawake.
Katika kukamilisha hayo yote Chama cha Wanawake wanasheria Tanzania TAWLA kwa kushirikiana na asasi mbalimbali wamezindua kampeni juu ya kutetea haki za watoto walioko magerezani na wenye kesi mahakamani kwa kutumia sheria zitazoweza kuwapatia haki zao pamoja na matunzo ya afya na elimu wawapo magerezani.
Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria Wanawake Tanzania Bi. MARIA KASHONDE amesema kuwa kampeni hizo zitasaidia watoto waliofungwa na mama zao magerezani kwa kukosa watu wakuwatunza watoto hao ili waweze kupata dhamana ikiwa pamoja na kufungwa vifungo vya nje.
No comments:
Post a Comment