MWANAMUZIKI maarufu wa bendi kongwe ya Msondo ngoma, Muhidin Gurumo aliyelazwa Hospital ya Taifa Muhimbili kwa ugunjwa wa shinikizo la Damu anaendelea vizuri.
Akizungumza na Dar es Salaam jana,Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'SUPER D'alisema afya ya GURUMO inaendelea vizuri na wakati wowote ataruhusiwa kutoka hospitalini hapo.
Alisema kuwa madaktari wanataka kuchukua vipimo vya mwisho kwa kina kujua kila kitu kinachomsumbua katika mwili wake.
"Kwa sasa tunashukuru Mungu afya ya Gurumo inaendelea vizuri tofauti na mara ya kwanza na akiendelea hivi anaweza kuruhusiwa hivi karibuni"alisema SUPER D.
No comments:
Post a Comment